Thursday, July 22, 2010

Wakazi wa kunduchi mtongani wafunga barabara!!


Mzozo umeibuka baina ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wanaoishi eneo la Kunduchi Mtongani na askari wa kikosi cha kutuliza ghasia - FFU katika harakati za askari hao kuwaondoa barabarani baada ya wakazi hao kuzuia magari kwa magogo na mawe wakidai barabara hiyo iwekwe matuta. Kutokana na vurugu hizo baadhi ya wakazi hao walijikuta wakikumbana na kipigo kutoka kwa askari hao ambao baada ya kipigo waliwaingiza ndani ya gari la polisi. Hata hivyo baadhi ya wakazi hao walipohojiwa sababu ya azma yao ya kuzuia magari wamesema uamuzi huo umekuja baada ya kugongwa kwa mwanafuzi wa darasa la pili jana ambaye alikufa papo hapo katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment